ATCL: Ndege zetu zipo salama

LNa Nora Damian, Mtanzania Digital Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limewatoa hofu Watanzania na kusema ndege zake ziko salama na hitilafu iliyotokea hivi karibuni ni ya kawaida. Ndege ya Airbus A 220 – 300 ambayo ilikuwa ikielekea Mbeya ililazimika kujerea Dar es Salaam kutokana na hitilafu iliyotokea katika moja ya injini zake. Akizungumza Februari 29,2024 […]

Mar 1, 2024 - 06:00
 0
ATCL: Ndege zetu zipo salama

LNa Nora Damian, Mtanzania Digital

Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limewatoa hofu Watanzania na kusema ndege zake ziko salama na hitilafu iliyotokea hivi karibuni ni ya kawaida.

Ndege ya Airbus A 220 – 300 ambayo ilikuwa ikielekea Mbeya ililazimika kujerea Dar es Salaam kutokana na hitilafu iliyotokea katika moja ya injini zake.

Akizungumza Februari 29,2024 na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladslaus Matindi, amesema hitilafu hiyo ilikuwa ndogo na ya kawaida.

Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladslaus Matindi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hitilafu iliyotokea katika moja ya ndege za shirika hilo.

“Injini moja ilipata joto na ikawa na mafuta mengi ndiyo yaliyosababisha moshi ambao uliingia kwenye mifumo ya hewa na kuwafikia abiria lakini si ndege kuungua moto kama ilivyoelezwa.

“Hali haikuwa ya kutisha na marubani na wahudumu walijitahidi kuchukua hatua za kiusalama kwa kuwapa taarifa abiria na kuwasihi wasiwe na wasiwasi,” amesema Matindi.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, hitilafu hiyo ilidumu kwa dakika tano kisha ndege ilirudi Dar es Salaam na abiria walibadilishiwa ndege nyingine na kuendelea na safari.

Naye Mkuu wa Usalama wa ATCL, Emmanuel Tivai, amesema hitilafu iliyotokea ni ya kawaida kwa vyombo vya usafiri na kwamba wahandisi wanaendelea kufanya uchunguzi.

Mmoja wa wahudumu aliyekuwepo katika ndege hiyo, Mwanaidi Mwanga, amesema mafunzo ya usalama waliyoyapata yaliwawezesha kudhibiti taharuki iliyokuwa imetokea.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.