CNG ipewe kipaumbele kuendesha mitambo na magari nchini –Kamati ya Bunge

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeishauri Serikali kuweka kipaumbele katika kusambaza Vituo vya Nishati ya Gesi Iliyoshindiliwa (CNG) inayotumika katika kuendesha mitambo na magari nchini ili kukabiliana na gharama za mafuta pale zinapotokea. Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 18, 2023  jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati […]

Oct 18, 2023 - 10:00
 0
CNG ipewe kipaumbele kuendesha mitambo na magari nchini –Kamati ya Bunge

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeishauri Serikali kuweka kipaumbele katika kusambaza Vituo vya Nishati ya Gesi Iliyoshindiliwa (CNG) inayotumika katika kuendesha mitambo na magari nchini ili kukabiliana na gharama za mafuta pale zinapotokea.

Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 18, 2023  jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Mathayo David wakati Kamati hiyo ilipopokea taarifa ya Wizara ya Nishati, kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa kuanzisha vituo hivyo.

“Tunashauri Serikali iweke kipaumbele katika matumizi ya gesi asilia katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na matumizi mengine ili Watanzania waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi,” amesema Mwenyekiti wa Kamati,  Mathayo David.

Katika hatua nyingine, Mathayo ameipongeza Serikali kwa mikakati mizuri ya uanzishwaji wa karakana za kubadili mifumo ya matumizi kutoka kwenye mafuta na kwenda kwenye gesi asilia kwenye magari hali  inayochochea matumizi ya gesi asilia nchini kwa wingi.

“Uwepo wa karakana hizi kwa wingi utarahisisha utoaji wa huduma za ubadilishaji mifumo na ukarabati wa hitilafu kwa muda mfupi na karakana hizi zitumie teknolojia ya kisasa wakati wa kubadili magari na mitambo,” ameeleza Mathayo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema Serikali imepokea ushauri wote uliotolewa na kamati ili kuweza kuboresha Sekta ya Nishati nchini. 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko.

Amesema, Wizara imedhamiria kuchochea matumizi ya Gesi Asilia iliyoshindiliwa kwa maeneo pia  yaliyo mbali na mtandao wa mabomba pamoja na matumizi ya gesi hiyo kwenye magari kwa kuwa na vituo vingi vya kujazia gesi kwenye magari.

Viongozi mbalimbali walioshiriki katika kikao hicho ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Innocent Luoga na Watendaji kutoka Wizara na Taasisi.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.