Dhibitini mienendo yote inayohatarisha amani Kalambo- DC Komba

Na Grace Mwakalinga, Mtanzania Digital MKUU wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Lazaro Komba, ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo, kuhakikisha vinadhibiti mienendo yote inayolenga kuhatarisha ustawi wa watoto wakiwemo wenye ualbino katika jamii. Komba alitoa kauli hiyo jana wakati wa kujadili masuala ya kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto ili utu na […]

Jun 25, 2024 - 19:00
 0
Dhibitini mienendo yote inayohatarisha amani Kalambo- DC Komba

Na Grace Mwakalinga, Mtanzania Digital

MKUU wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Lazaro Komba, ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo, kuhakikisha vinadhibiti mienendo yote inayolenga kuhatarisha ustawi wa watoto wakiwemo wenye ualbino katika jamii.

Komba alitoa kauli hiyo jana wakati wa kujadili masuala ya kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto ili utu na heshima zao vizingatiwe kama watu wenye haki ya kuishi.

Alisema imani potofu zimesababisha watoto wenye ulemavu hususani wenye ualbino kufanyiwa ukatili kama vile kuuawa na kunyofolewa baadhi ya viongo kwenye miili yao.

Kutokana na suala hilo ambalo limeripotiwa katika baadhi ya maeneo nchini, Lazaro alisema tayari wilaya ya Kalambo imeanza kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kuweka mikakati kuanzia ngazi ya kitongoji kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kuthibiti vitendo hivyo.

“Ulinzi na usalama kwa watoto wenye mahitaji maalum ni jukumu la kila mmoja wetu, tushiriki kuhakikisha wanalindwa dhidhi ya ubaguzi, unyanyasaji na ukatili wa aina zote ikiwemo mauaji ya watoto wenye Ualbino,” alisema Komba.

Aliongeza kuwa tayari baadhi ya wadau wanaendelea kutekeleza jukumu la ulinzi na usalama wa watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo wenye ualbino ambao ni Child Support Tanzania (CST), kukemea na kupinga ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye Ualbino yaliyoripotiwa hivi karibuni likidai vitendo hivyo vinajenga hofu na kutishia usalama kwa makundi hayo.

Mratibu wa CST, Nemes Temba alisema wananchi wanapaswa kuachana na Imani potofu dhidi ya watu wenye ualbino kwa madai kuendeleza Imani hizo ni kwenda kinyume na maagizo ya vitabu vitakatifu, katiba ya nchi na mikataba mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo inasisizita haki ya kuishi kwa kila mtu bila kujali hali aliyonayo.

Aliongeza kuwa jukumu la jamii ni kufungua fursa za kielimu na kuweka mazingira rafiki kwa watoto wenye mahitaji maalum ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao.

“Tulikuwa na maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika hapa mkoani Rukwa ambayo ilikuwa mahsusi kujadili na kuangali masuala ya kuyatekeleza kuhakikisha ulinzi na usalama kwa watoto wenye mahitaji maalum.

Miongoni mwa miradi tunayotekeleza ni kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapelekwa shule kuanza masomo, uboreshwaji wa miundombinu ya shule jumuishi zilizopo mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi kuwapatia vifaa vya kufundishia na kujifunzia, madarasa na vifaa vyao vya usaidizi kulingana na ulemavu wa kila mmoja.

“ Kauli mbinu ya mtoto wa Afrika mwaka huu inazungumzia Elimu Jumuishi kwa watoto izingatie maadili na maarifa na stadi za maisha inahimiza jamii kutoa elimu yenye usawa kwa watoto wote, wenye ulemavu na wasio na ulemavu,” alisema Temba.

Aliongeza kuwa katika kufanikisha program za ulinzi na usalama kwa watoto wenye mahitaji Wizara ya Shirikisho ya Ushirikiano wa Kiuchumina Maendeleo ya Ujelumani (BMZ) kwa kushirikiana na asasi ya Christian Blind Mission (CBM) wametoa ufadhili kwa mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.