FCS yatoa tathimini ya Mwaka mmoja utekelezaji mradi wa ‘URAIA WETU’

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Foundation For Civil Society (FCS), kupitia mradi wake wa ‘Uraia Wetu’ imeendelea kuweka nia ya kuchangia, kuboresha, na kuwezesha mfumo wa sera na mazingira ya ushirikishwaji wa wananchi ili kukuza utawala wa Demokrasia nchini. Malengo makubwa ya Mradi huo ni kukuza uhuru wa kujieleza, kupata habari, uhuru wa kukusanyika na […]

Dec 19, 2023 - 16:00
 0
FCS yatoa tathimini ya Mwaka mmoja utekelezaji mradi wa ‘URAIA WETU’

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Foundation For Civil Society (FCS), kupitia mradi wake wa ‘Uraia Wetu’ imeendelea kuweka nia ya kuchangia, kuboresha, na kuwezesha mfumo wa sera na mazingira ya ushirikishwaji wa wananchi ili kukuza utawala wa Demokrasia nchini.

Malengo makubwa ya Mradi huo ni kukuza uhuru wa kujieleza, kupata habari, uhuru wa kukusanyika na kubaini fursa na nafasi iliyopo kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika masuala ya kiraia.

Msimamizi wa Mradi wa ‘Uraia Wetu’ Nicholas Lekule akitoa tathimini juu ya Mradi huo, katika semina ya Wahariri na Waandishi wa Habari iliyofanyika Desemba 18,2023 jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa Mradi wa ‘Uraia Wetu’ Nicholas Lekule, alipokuwa akitoa tathimini juu ya Mradi huo katika semina ya Wahariri na Waandishi wa Habari iliyofanyika Desemba 18,2023 jijini Dar es Salaam.

“Lengo la mradi huu wa miaka mitatu, ni kuwa asasi za kiraia ambazo zimeratibiwa vizuri kuanzia katika masuala ya kisheria, kisera na utekelezaji, ili kazi zinazofanywa ziwe na ufanisi mzuri,” amesema Lekule.

Sehemu ya washiriki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MTWANGO NET, Fidea Ruanda, ameishukuru FCS kwa kutoa ruzuku ya kutekeleza Mradi huo wanaotekeleza kwa miaka mitatu katika mikoa saba ikiwemo Songwe, Ruvuma, Iringa, Njombe, Mbeya, Mtwara, Rukwa, ambapo wanasimamia Kanda ya kusini na kwamba unaolenga kuwajengea uwezo vijana, wanawake, na walemavu.

“Uwelewa mdogo kuhusu sera, sheria na miongozo mbalimbali ikiwemo kulipa ada kwa mashirika machanga bado ni changamoto licha ya kuwa malipo ni shilingi 50,000 kwa mwaka kwani usipolipa hadi kufikia mwezi wa April mwaka unaofuata unapigwa faini asilimia 100 ambapo ni sawa na shilingi 100,000,” amesema Fidea.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.