JKT kuunganisha vijana BBT

*Ni wale wanaohitimu mafunzo ya JKT Na Ramadhan Hassan, Dodoma JESHI la Kujenga Taifa (JKT) lipo katika mkakati wa mazungumzo na Wizara za Kilimo na ile ya Mifugo na Uvuvi ili kuwaunganisha vijana ambao wamemaliza mafunzo ya JKT na hawana kazi katika mradi wa Building Better Tomorrow (BBT). Hayo yameelezwa leo Julai 27,2023 na Mkuu […]

Jul 27, 2023 - 17:00
 0
JKT kuunganisha vijana BBT

*Ni wale wanaohitimu mafunzo ya JKT

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) lipo katika mkakati wa mazungumzo na Wizara za Kilimo na ile ya Mifugo na Uvuvi ili kuwaunganisha vijana ambao wamemaliza mafunzo ya JKT na hawana kazi katika mradi wa Building Better Tomorrow (BBT).

Hayo yameelezwa leo Julai 27,2023 na Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Rajabu Mabele wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo kwa mwaka 2023-2024 kwa Waandishi wa Habari.

Meja Jenerali Mabele amesema wapo katika mazungumzo na wizara hizo kuhakikisha vijana wanaomaliza Jeshi wanajiunga katika mpango huo.

Amesema kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha vijana wengi wanapatiwa mafunzo na Jeshi hilo  ambayo yatawasaidia kuwa na malezi bora ya kizalendo kwa manufaa ya  nchi yao.

“Tunamshukuru sana Rais wetu kwa nia ya dhati katika kuliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa JKT ambapo bajeti imeongezeka  kwa asilimia 54 toka Sh bilioni 3.7 kwa mwaka 2021/2022 hadi kufikia bajeti ya sh bilioni 9.96 kwa Mwaka 2023/2024,” amesema.

Amesema fedha hizo pia zitatumika kuboresha vyuo vya ufundi vya Jeshi hilo kwa lengo la kuwapatia vijana ujuzi na maarifa pale wanapokuwa wanapatiwa mafunzo ili kuweza kujitegemea na kujiajiri.

Pia amesema jeshi hilo limejipanga katika suala zima la uzalishaji ikiwemo kilimo na ufugaji ili Tanzania kuweza kuwa ghala la chakula.

“Sisi kama Jeshi katika mwaka huu wa fedha tumejipanga kujenga miundombinu ya  Skimu za umwagiliaji ambapo  mradi huo umetengewa jumla ya Shilingi bilioni4 katika kukidhi hitajio la chakula ili nchi iwe na usalma wa chakula,” amesema Meja Jen. Mabele.

Amesema wataongeza idadi ya uzalishaji wa mpunga kutoka ekari 3,000 hadi 5,000 huku mahindi kutoka ekari 6,625 hadi 8,500 na kuweza kupata tani 12,750 na alizeti kutoka ekari 2,115 hadi 6,000.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.