Kamati ya Bunge ya Ardhi yampongeza Rais Samia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Timotheo Mzava wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzisha Mfumo wa Unganishi wa Teknolojia ya Usimamizi wa Sekta ya […]

Jan 8, 2024 - 18:00
 0
Kamati ya Bunge ya Ardhi yampongeza Rais Samia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Timotheo Mzava wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzisha Mfumo wa Unganishi wa Teknolojia ya Usimamizi wa Sekta ya Ardhi.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyotembelea timu ya wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inayoandaa mfumo huo jijini Arusha iliyofanyika Januari 8, 2024.

Mzava ameipongeza Wizara ya Ardhi kwa kazi kubwa na nzuri na kueleza kuwa kazi hiyo inakwenda kuacha alama kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha uongozi kwa kuiacha sekta ya ardhi katika mifumo bora.

“Nichukue fursa hii kumpongeza Mhe Rais kwa kazi hii nzuri, kama kamati wameridhishwa na kazi na hongereni sana na mfumo huu uende ukawe bora na kutoa huduma kwa watanzania,” alisema Mzava.

Baadhi ya wabunge wamesema mfumo huo siyo tu utarahisisha na kuharakisha huduma za sekta ya ardhi bali utajibu maswali mengi yakiwemo ya kijamii.

“Niipongeze wizara ya ardhi kwa kufanyia kazi mfumo utakaojibu maswali mengi ya kijamii na ningetamani mfumo huu ungejibu maswali na changamoto za kiuchumi,” alisema Lucy Mayenga mbunge wa viti Maalum.

Mbunge wa Makete mkoani Njombe, Festo Sanga aliipongeza Wizara kwa kuboresha mfumo na kueleza kuwa uboreshaji huo umechelewa ingawa uko katika hatua nzuri.

Hata hivyo, mbunge huyo wa Makete alitaka kufahamu utayari wa wizara ya Ardhi katika kutumia mfumo hususan kwenye eneo la usalama wa mifumo.

Naye, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema mfumo huu unganishi wa usimamizi wa sekta ya ardhi utarahisisha utowaji wa huduma za sekta ya ardhi kwa mtandao bila kufika ofisi za Ardhi na unatarajiwa kuanza katika mikoa mitano ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Tanga.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.