Majaliwa mgeni rasmi miaka 10 ya Maendeleo Benki

*Yatangaza gawio la milioni 700 kwa wanahisa Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuwa Mgeni rasmi kwenye kusherekea miaka 10 ya Maendeleo Banki tangu kuanzishwa kwa benki hiyo kufanyika Septemba 2, mwaka huu katika viwanja vya Farasi jijini Dar es Salaam. Hayo yamebainishwa Agosti 9, jijini Dar es Salaam wakati akitangaza […]

Aug 10, 2023 - 16:30
 0
Majaliwa mgeni rasmi miaka 10 ya Maendeleo Benki

*Yatangaza gawio la milioni 700 kwa wanahisa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuwa Mgeni rasmi kwenye kusherekea miaka 10 ya Maendeleo Banki tangu kuanzishwa kwa benki hiyo kufanyika Septemba 2, mwaka huu katika viwanja vya Farasi jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa Agosti 9, jijini Dar es Salaam wakati akitangaza gawio kwa wanahisa la Sh milioni 708 kwa mwaka wa fedha 2022 na Mkuu wa Usimamizi wa Athari na Taratibu za Benki wa Benki hiyo, Peter Tarimo ambapo amesema mkutano wa tisa wa wanahisa uliofanyika Juni 24, mwaka huu walipitisha kwa kauli moja mapendekezo na Bodi ya Wakurugenzi kuhusu malipo ya gawio la Sh 26 kwa kila hisa.

Amesema jumla ya gawio la milioni 708 hiyo ikiwa ni ongezeko la asilimia 136 ikilinganishwa na gawio la Sh 11 kwa hisa la mwaka 2021.

“Benki inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake na katika kusheherekea imeaandaa mbio “Maendeleo Banki Marathon” na fedha zitakazopatikana zitapelekwa hospitali ya KCMC kwa ajili ya watoto njiti na kituo cha watoto wenye usonji kilichopo Mtoni Mtongani hapa Dar es Salaam na kauli mbiu ya mbio hizi ni ‘Hatua ni faraja‘,” amesema Tarimo.

Amesema gawio hilo ni mgawo wao wa nne na wa pili kwa pesa taslimu tangu kuanzishwa kwa benki mwaka 2013 hivyo inaonyesha dhamira ya benki ya kuwatunza wenyehisa kwa umiliki wao.

Tarimo amesema benki hiyo ina malengo ya mikakati ni kuwa benki ya kitaifa kwa kufungua matawi mbalimbali nakwamba watafikia azima hiyo ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.

Aidha, amesema wanawataarifu kuwa gawio kwa wanahisa litalipwa Oktoba 6, mwaka huu kwa wanahisa wote watakuwa kwenye usajili wa wanahisa Agosti 31, mwaka huu na kwamba waendelee kuwekeza katika benki hiyo.

Naye Meneja Usajili Hisa na Hati Fungani kutoka Kampuni ya Uhifadhi Dhamana (CSDR), Gidion Kapange amesema changamoto kubwa wanahisa hawaleti taarifa mapema wapate gawio lao.

“Takwimu zinaonyesha asilimia 60 wamechukua gawio na asilimia 60 bado kuchukua gawio kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo account zao wamekosea wengine zipi domati hawajatumia mda mrefu na elimu inahitajika kwa wanahisa,” amesema Kapange.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.