Matumizi ya maudhui ya ndani sekta ya ujenzi kuchochea ukuaji uchumi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) umesema, matumizi ya maudhui ya ndani katika sekta ya ujenzi itaongeza ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini nchini. Maudhui ya ndani yanarejelea matumizi ya makampuni ya ndani, wataalam binafsi, nyenzo zinazopatikana nchini na utaalamu katika kuendeleza miradi ya ujenzi. “Kutengeneza fursa kwa wananchi wa eneo […]

Oct 11, 2023 - 08:00
 0
Matumizi ya maudhui ya ndani sekta ya ujenzi kuchochea ukuaji uchumi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) umesema, matumizi ya maudhui ya ndani katika sekta ya ujenzi itaongeza ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini nchini.

Maudhui ya ndani yanarejelea matumizi ya makampuni ya ndani, wataalam binafsi, nyenzo zinazopatikana nchini na utaalamu katika kuendeleza miradi ya ujenzi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mohamed Besta.

“Kutengeneza fursa kwa wananchi wa eneo husika kujipatia kipato kupitia kuajiriwa ni miongoni mwa njia za kupunguza umaskini.

“Mchakato wa kujenga, kuendesha na kutunza miundombinu unatoa fursa kubwa kwa ajili ya kutengeneza ajira na kuna maelewano mapana miongoni mwa Watanzania katika kuongeza fursa hizi,” alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mohamed Besta, mapema wiki hii.

Besta alisema Kutegemea makampuni ya kigeni kubuni na kutengeneza vifaa si jambo endelevu, kwani utaalamu unaweza kukoma pindi ujenzi unapokamilika.

Tanroads inasimamia mtandao wa barabara zenye urefu wa kilomita 36,760.29 ikiwa na jukumu la kuboresha barabara ikiwemo kwenye viwanja vya ndege.

Mwongozo wa Kitaifa wa Maudhui ya Sekta Mbalimbali za Mitaa uliotolewa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (2019) umebainisha kuwa sekta ya ujenzi inayopewa kipaumbele katika kuendesha ajenda ya maudhui ya ndani nchini.

Baadhi ya hatua zinazochukuliwa na serikali kukuza maudhui ya ndani katika sekta ya ujenzi na sekta nyinginezo ni pamoja na kutunga sheria na kanuni zinazohitaji makampuni ya ujenzi kuweka kipaumbele cha maudhui ya ndani katika miradi yao, kujenga uwezo wa wataalam wa ndani, kuhimiza makampuni ya ndani ya ujenzi na huduma kushindana katika miradi ya miundombinu ya ukubwa na ugumu mbalimbali, na kukuza ubia kati ya makampuni ya ndani na nje ya nchi.

Bodi ya Wakandarasi (CRB) pia ina utaratibu wa kufadhili kupitia Mfuko wa Msaada wa Wakandarasi (CAF), ambao unalenga kuwawezesha wakandarasi wa ndani kupata miradi zaidi.

Hazina hiyo ilidhamini miradi 236 yenye thamani ya jumla ya Sh bilioni 129.95 mwaka wa 2022 ili kusaidia wakandarasi kwa malipo ya awali ya jumla ya Sh bilioni 14.78, kulingana na bodi hiyo.

Jambo ambalo limesaidia hivi majuzi wakandarasi wa ndani na washauri kushinda zabuni za serikali za umma ni kuzingatia upya, uwazi, na usaidizi katika mchakato wa ununuzi.

Kulingana na tovuti ya Statistica, Sekta ya ujenzi ilichangia Sh trilioni 15 kwenye pato la Taifa kutoka robo ya kwanza hadi ya tatu ya 2021. Mwaka 2020, thamani ya sekta hiyo katika uchumi ilifikia Sh trilioni 19.4 ikiwa ni kiwango cha juu zaidi tangu 2015.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka huu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), zinaonyesha kuwa pato la Taifa la Tanzania limeongezeka hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 85.42 (Sh trilioni 200) kwa mwaka huu 2023 kutoka Dola za Marekani Bilioni 69.9 (Sh trilioni 163.5) mwaka 2021.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.