NCAA yazitaka baadhi ya taasisi kuacha upotoshaji kuhusu wanaohama kwa hiari

Na Mwandishi wetu Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imezitaka baadhi ya taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka ndani na nje ya nchi kuacha upotoshaji kuhusiana na zoezi la kuhamisha wananchi kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro wanaojiandikisha kwa hiyari kwenda Kijiji cha Msomera na badala yake kutafuta ukweli kuhusu suala hilo. […]

Jun 24, 2024 - 22:00
 0
NCAA yazitaka baadhi ya taasisi kuacha upotoshaji kuhusu wanaohama kwa hiari

Na Mwandishi wetu

Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imezitaka baadhi ya taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka ndani na nje ya nchi kuacha upotoshaji kuhusiana na zoezi la kuhamisha wananchi kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro wanaojiandikisha kwa hiyari kwenda Kijiji cha Msomera na badala yake kutafuta ukweli kuhusu suala hilo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa tamasha la jamii ya wamasai lililofanyika ndani ya hifadhi ya Ngorongoro Kaimu Meneja wa Uhusiano kwa umma wa mamlaka hiyo Hamis Dambaya amesema baadhi ya taasisi zimekuwa zikiripoti kwamba kabila la wamasai wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo wamekuwa wakifukuzwa na kuondolewa kwa nguvu kitu ambacho si cha kweli na ndio maana hata tamasha hilo lililofanyika ndani ya kreta ya Ngorongoro kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo watumishi NCAA ilitoa kibali.

Amesema jamii ya kimasai, wahadzabe, wamang’ati wanaoishi ndani ya hifadhi imekuwa na ushirikiano mkubwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ndiyo maana zoezi la uelimishaji wa wananchi kuhama kwa hiyari limekuwa likifanyika bila upinzani wowote hivyo ni vema taasisi hizo kuacha kuipotosha dunia.

“Matamasha na sherehe kama hizi mamlaka huyatumia kama sehemu ya kuja kutoa elimu kwa wananchi katika njia ya makundi ama mtu mmoja mmoja na hizi ni salamu tosha kwa mashirika ya kimataifa yanayodai kuwa Tanzania inawaondoa wamasai kwa nguvu katika maeneo yao”.Kaimu Meneja huyo wa uhusiano kwa umma amesema,

Ameeleza kuwa katika tamasha hilo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliweza kuwaelimisha wananchi mmoja mmoja ama kwa makundi kuhusu huduma za kijamii ambazo serikali inazitoa katika Kijiji cha Msomera ukilinganisha na maisha ya ndani ya hifadhi na baadhi ya wananchi kusema kuwa wapo tayari kuondoka katika eneo hilo kuwafuata wenzao waliotangulia.

Kauli hiyo ya kaimu Meneja wa Uhusiano kwa Umma imetolewa kuzijulisha baadhi ya taasisi za kimataifa ikiwemo ile inayojiita Masaai International Solidarity Alliance, Kitengo cha kutetea Haki za binadamu cha Chuo Kikuu cha Pretoria na Jarida la Africa Intelligence ambapo katika siku za hivi karibuni walitoa taarifa kwamba kuna uondoaji wa kutumia nguvu wa wamasai katika maeneo yao jambo ambalo sio la kweli.

Dambaya amesema tuhuma hizo zina upotoshaji mkubwa kwani katika jamii inayozunguka nchi nzima kutafuta malisho na maeneio ya kuchungia hakuna mwananchi hata mmoja katika nchi hii aliyewahi kubughudhiwa kutoka eneo lake ama sehemu aliyoamua kuhamia.

“Tanzania hakuna sehemu ambayo jamii ya wafugaji wanasumbuliwa au kuondolewa kwa nguvu na ndiyo maana wameenea kila kona kuanzia bara hadi visiwani sasa anapotokea mtu na kudai kuwa mmasai anahamishwa kwa nguvu tena shirika hilo likidai ni la kutetea wamasai labda wanaoongoza shirika hilo ni wamasai wa nchi nyingine duniani lakini hawa wa hapa nchini wanaujua ukweli na hakuna mtu anayewabughudhi”.alisema Dambaya.

Katika tamasha hilo vijana wa kimasai wakiongozwa na wazee wa mila walifanya matambiko yao ya kimila ambapo walisema zoezi kama hilo hata wakiamua kuhamia sehemu yoyote ile duniani wanaweza kuendelea kulifanya bila athari yoyote ambapo pia baadhi ya wageni waliotembelea kreta waliweza kuwashuhudia jamii hiyo ikishiriki tamasha hilo.

Baadhi ya mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yamekuwa yakipotosha kuhusu zoezi la kuhamisha watu kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kwenda Msomera kutokana na wengi wa watetezi hao kusikiliza taarifa za watu wachache wanaowatumia wananchi wa jamii hiyo kuweza kupata kipato kupitia baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yamekuwa yakipokea fedha kwa madai ya utetezi wa haki za binadamu.

Serikali ya Tanzania inaendelea na zoezi la kuhamisha wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi ya Ngorongorowanaojiandikisha kuhama kwa hiyari ili kuweza kuwanusuru wananchi hao kutokana na ugumu wa maisha na kwenda sambamba na kutimiza malengo ya milenia yanayosisitiza juu ya usalama wa watu na maisha bora kwa wote.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.