Rais wa Algeria afanya mazungumzo na Dk. Tax

Na Mwandishi Wetu, Algeria Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune amekutana Kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax (Mb.) alipomtembelea Ikulu Jijini Algiers, Algeria tarehe 1 Agosti 2023. Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya […]

Aug 1, 2023 - 19:30
 0
Rais wa Algeria afanya mazungumzo na Dk. Tax

Na Mwandishi Wetu, Algeria

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune amekutana Kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax (Mb.) alipomtembelea Ikulu Jijini Algiers, Algeria tarehe 1 Agosti 2023.

Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Algeria ulioanza Julai 30 hadi Agosti mosi, 2023.

Mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kirafiki na kidiplomasia ili kuweza kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa maslahi mapana ya nchi zao.

Aidha, katika kuendelea kuimarisha ushirikiano Waziri Tax pamoja na majukumu mengine, atafanya ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 2, 2023 jijini Algiers.

Ufunguzi rasmi wa ofisi za ubalozi huo ni hatua muhimu hasa wakati huu ambapo viongozi hao wamekubaliana kuinua sekta za uchumi ambazo ni pamoja na biashara.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune amekutana Kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax (Mb.) alipomtembelea Ikulu Jijini Algiers, Algeria Agosti mosi 2023.

Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Algeria unaofanyika kuanzia Julai 30 hadi Agosti mosi, 2023.

Mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kirafiki na kidiplomasia ili kuweza kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa maslahi mapana ya nchi zao.

Aidha, katika kuendelea kuimarisha ushirikiano Mhe. Waziri, Dk. Tax pamoja na majukumu mengine, atafungua rasmi Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 2,2023 jijini Algiers.

Ufunguzi rasmi wa ofisi za ubalozi huo ni hatua muhimu hasa wakati huu ambapo viongozi hao wamekubaliana kuinua uchumi kupitia sekta za biashara, uwekezaji, nishati, madini, elimu, sayansi na teknolojia, afya na utalii.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.