REA yatenga Bilioni 10 kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia

Na Mwandishi wetu,Dodoma WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) kwa mwaka 2023-24 umetenga jumla ya Sh bilioni 10 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia. Hayo yameelezwa leo Ijumaa Agosti 18,2023 na Mkurugenzi Mkuu REA, Hassan Saidy wakati akieleza utekelezaji wa miradi ya REA kwa mwaka 2023-2024 na mwelekeo wa Wakala […]

Aug 18, 2023 - 12:00
 0
REA yatenga Bilioni 10 kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia

Na Mwandishi wetu,Dodoma

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) kwa mwaka 2023-24 umetenga jumla ya Sh bilioni 10 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Agosti 18,2023 na Mkurugenzi Mkuu REA, Hassan Saidy wakati akieleza utekelezaji wa miradi ya REA kwa mwaka 2023-2024 na mwelekeo wa Wakala huo.

Mkurugenzi huyo amesema Wakala unatumia utaratibu wa utoaji ruzuku kuwezesha usambazaji wa mitungi ya gesi ya kupikia (LPG) 71,000 yenye thamani ya Sh bilioni 3 pamoja na majiko banifu 200,000 katika maeneo ya vijijini.

Amesema kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 Sh bilioni 10 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha mradi huo.

Amesema Serikali imepanga kufikisha umeme katika vitongoji ili kuhakikisha kuwa umeme unafika na kutumika maeneo ya vijijini Tanzania Bara.

Amesema Serikali kupitia REA ilifanya utambuzi wa wigo wa mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji vyote Tanzania Bara na kubaini kuwa vitongoji ambavyo bado havijafikiwa na miundombinu ya umeme nchini ni 36,101 kati ya vitongoji 64,760 vilivyopo Tanzania Bara.

Aidha, gharama za kufikisha miundombinu ya umeme katika vitongoji hivyo (36,101) ni Sh trilioni 6.7.

Amesema Serikali ilipata mkopo wa gharama nafuu kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kupitia dirisha la Extended Credit Facility ambapo kiasi cha Shilingi bilioni 100 zitatumika kuanza utekelezaji wa mradi huo katika vitongoji 654.

Miradi hiyo ni katika mikoa ya Songwe na Kigoma na hivyo kufanya vitongoji ambavyo havina umeme kuwa 36,101.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.