Serikali, wananchi waombwa kumsaidia kijana Elia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Shule ya Msingi Lusasaro iliyoko Tabata Kisukuru jijini Dar es Salaam imewaomba Watanzania na Serikali kwa jumla kumsaidia mtoto yatima, Elia Hubert (14) aliyemaliza shuleni hapo. Mwalimu wa Taaluma wa Shule hiyo, Maganiko Simon anasema kwamba shule yake imemsomesha mtoto huyo bure elimu ya msingi na kuweza kufaulu vizuri na […]

Dec 31, 2023 - 00:00
 0
Serikali, wananchi waombwa kumsaidia kijana Elia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shule ya Msingi Lusasaro iliyoko Tabata Kisukuru jijini Dar es Salaam imewaomba Watanzania na Serikali kwa jumla kumsaidia mtoto yatima, Elia Hubert (14) aliyemaliza shuleni hapo.

Mwalimu wa Taaluma wa Shule hiyo, Maganiko Simon anasema kwamba shule yake imemsomesha mtoto huyo bure elimu ya msingi na kuweza kufaulu vizuri na kuchaguliwa kujiunga shule ya serikali ya kutwa ya Bagozalakini changamoto ni uwezo duni wa familia yake ambayo haiwezi kumudu gharama za elimu za kijana huyo.

“Naiomba serikali imsaidie ikiwamo kumpangia shule ya bweni na pia nawaomba Watanzania wamchengie kijana fedha za kumuwezesha kumudu gharama mbalimbali za elimu kupitia namba 0756 729 019 majina ya Mpokeaji ni Joyce Ngalula,” amesema Simon.

Naye mama Mlezi wa Kijana huyo, Saada Hussein anawaomba Watanzania wamchangie kijana huyo ili aweze kumudu gharama za elimu huku akiiomba serikali impangie kijana huyo shule ya bweni kwani familia yake haina uwezo hata wa kumpa nauli na malazi kijana huyo ikiwamo nauli za kila siku.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.