Serikali yasitisha zoezi la ukaguzi wa risiti soko la Kariakoo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital SERIKALI imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi  iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, jijini  Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo. Hayo yamesemwa kwa […]

Jun 24, 2024 - 19:00
 0
Serikali yasitisha zoezi la ukaguzi wa risiti soko la Kariakoo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

SERIKALI imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi  iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, jijini  Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.

Hayo yamesemwa kwa niaba ya Serikali, leo Juni 24,2024 jijini Dodoma, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na kuhudhiriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.