Serikali yaweka mikakati kuondoa foleni ya malori Tunduma

Na Mwandishi Wetu, Tunduma Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara amewahakikishia wadau wanaotumia Kituo cha Forodha Tunduma mkoani Songwe kuvusha mizigo kupitia Nakonde upande wa Zambia kuwa changamoto zilizopo zinafanyiwa kazi. Kauli ya Prof. Kahyarara imekuja kufuatia maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zambia, Hakainde Hichelema kwamba watendaji wahakikishe […]

Sep 23, 2023 - 08:30
 0
Serikali yaweka mikakati kuondoa foleni ya malori Tunduma

Na Mwandishi Wetu, Tunduma

Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara amewahakikishia wadau wanaotumia Kituo cha Forodha Tunduma mkoani Songwe kuvusha mizigo kupitia Nakonde upande wa Zambia kuwa changamoto zilizopo zinafanyiwa kazi.

Kauli ya Prof. Kahyarara imekuja kufuatia maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zambia, Hakainde Hichelema kwamba watendaji wahakikishe changangamoto zote zinazowakabili wasafirishaji mizigo kwenda nchi za Zambia, DRC, Zimbabwe na nchi nyingine kuwa changamoto hizo zitatuliwa kwa haraka.

Prof. Kahyarara ameyasema hayo Septemba 23, 2023 kwenye kikao kilichowakutanisha Watendaji wa Serikali wanaofanya kazi katika mpaka wa Tunduma mkoani Songwe.

“Tayari taasisi ya Trade Mark East Afrika pamoja na Benki ya Dunia wako tayari kugharamia mpango kabambe wa maboresho mradi utakao gharimu dola milioni 27 na kutekelezwa kwa mwaka mmoja,” amesema Prof. Kahyarara.

Amesema mradi huo utakapokamilika utawezesha kituo hicho kuwa na mifumo inayosomana kwa kuwa na scanner za kisasa na kutumia mifumo ya kisasa ya TEHAMA, hatua itakayoongeza ufanisi na ushindani kwa Bandari ya Dar es Salaam.

“Hatua hiyo ni baadhi ya mageuzi makubwa yanayotekelezwa na Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuimarisha bandari na kukuza biashara na uchumi,’ amesema Prof. Kahyarara.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk. Francis Michael amesema pamoja na mkakati wa kuongeza upana wa barabara katika eneo hilo lakini bado kila mtu anayefanya kazi katika enao hilo ahakikishe anatimiza wajibu wake ili kuondoa msongamano wa malori.

Pia, Dk. Francis amesema kuwa Mkoa huo umejipanga kuanza kujenga bandari kavu eneo la Tunduma ili kuweza kupaki magari yote ambayo anasubilia kuvuka mpaka kwenda nchi jirani.

Naye Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoa wa Songwe, SSP Joseph Bukombe amesema kwasasa wameweka utaratibu wa kuvusha magari kwa awamu ili kupunguza foleni katika mpaka huo.

Mpaka wa Tunduma na Nakonde unakadiliwa kuvusha maroli zaidi ya elfu moja mia mbili kwa siku kutoka Tanzania kwenda Zambia, DRC Congo na Zimbabwe.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.