TANESCO kutumia 12 bilioni ujenzi kituo cha umeme Ushetu

Na Mwandishi wetu, Dodoma Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linatarajia kutumia kiasi fedha sh. 12 bilioni kwa ajili ya kujenga kituo kidogo cha umeme (Switching Station) kwenye Wilaya ya Ushetu eneo la Nyamirangano ili kuboresha hali ya upatikanaji wa nishati hiyo. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri […]

Nov 3, 2023 - 00:00
 0
TANESCO kutumia 12 bilioni ujenzi kituo cha umeme Ushetu

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linatarajia kutumia kiasi fedha sh. 12 bilioni kwa ajili ya kujenga kituo kidogo cha umeme (Switching Station) kwenye Wilaya ya Ushetu eneo la Nyamirangano ili kuboresha hali ya upatikanaji wa nishati hiyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, . Dk. Doto Biteko wakati akijibu swali la Mbunge wa Ushetu, Emmanuel Cherehani aliyeuliza, Je nini mkakati wa Serikali wa kupeleka umeme wa uhakika katika Halmashauri za Ushetu, Msalala, na Kahama?

Judith amesema pamoja na kituo hicho, TANESCO itaongeza njia nyingine za umeme kutokea kituoni hapo kwenda Ushetu, Msalala, na Kahama ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.

“Ujenzi wa mradi huu utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 12 na mradi unategemewa kukamilika katika mwaka wa fedha 2024/2025, “amesema Kapinga.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.