TARURA,TANROADS na Benki ya Dunia wakagua mradi wa ujenzi wa barabara

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff leo Julai 2,2024 ameshiriki katika ukaguzi wa mradi wa Ujenzi wa barabara ya Iringa – Kilolo akiambatana na TANROADS na ujumbe wa Benki ya Dunia. Mradi huo ni sehemu ya Mradi wa uboreshaji wa barabara vijijini […]

Jul 2, 2024 - 19:00
 0
TARURA,TANROADS na Benki ya Dunia wakagua mradi wa ujenzi wa barabara

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff leo Julai 2,2024 ameshiriki katika ukaguzi wa mradi wa Ujenzi wa barabara ya Iringa – Kilolo akiambatana na TANROADS na ujumbe wa Benki ya Dunia.

Mradi huo ni sehemu ya Mradi wa uboreshaji wa barabara vijijini na ufunguaji wa fursa za kiuchumi na kijamii unaotekelezwa na TARURA na TANROADS.

Ujumbe huo wa Benki ya Dunia unatembelea Miradi ya RISE kuona kama utekelezaji wake unaendelea kulingana na Mpango wa utekelezaji uliokubalika na kuona changamoto katika utekelezaji kama zipo.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa (Ipogolo)-Kilolo (33.61) ni wa kiwango cha lami unatekelezwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na Mkandarasi China Henan Engineering Company.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.