Ujenzi daraja Mto Majoka mbioni kukamilika

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Ujenzi wa daraja la Mto Majoka linalounganisha Mitaa ya Kifuru na Kibaga katika Kata ya Kinyerezi umefikia asilimia 60. Daraja hilo linalogharimu Sh milioni 650 fedha kutoka Serikali Kuu lilianza kujengwa Juni 2023 na linatarajiwa kukamilika Desemba, mwaka huu. Akizungumza Oktoba 5,2023 Mhandisi kutoka Tarura Wilaya ya Ilala, Legnard Mashanda, […]

Oct 7, 2023 - 13:00
 0
Ujenzi daraja Mto Majoka mbioni kukamilika

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Ujenzi wa daraja la Mto Majoka linalounganisha Mitaa ya Kifuru na Kibaga katika Kata ya Kinyerezi umefikia asilimia 60.

Daraja hilo linalogharimu Sh milioni 650 fedha kutoka Serikali Kuu lilianza kujengwa Juni 2023 na linatarajiwa kukamilika Desemba, mwaka huu.

Daraja la Mto Majoka linalounganisha Mitaa ya Kifuru na Kibaga katika Kata ya Kinyerezi, Dar es Salaam.

Akizungumza Oktoba 5,2023 Mhandisi kutoka Tarura Wilaya ya Ilala, Legnard Mashanda, amesema ujenzi utakamilika kabla ya muda uliopangwa.

Mashanda alikuwa akizungumza baada ya Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli, kufanya ziara kukagua ujenzi wa daraja hilo.

“Tumeendelea kumsimamia mkandarasi na tulitarajia daraja likamilike Desemba 26 lakini kwa kasi iliyopo tutakamilisha hata kabla ya muda uliopangwa,” amesema Mhandisi Mashanda.

Amesema kazi zilizobaki ni kuendelea kuufungua mto, kuchonga barabara na kuziwekea vifusi na ujenzi wa mitaro ya pembeni.

Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Leah Mgitu, amesema daraja hilo litakuwa na manufaa makubwa kwa kuunganisha mitaa ya Kifuru na Kibaga na kudhibiti mafuriko yaliyokuwa yakitokea awali.

Kwa upande wake Bonnah amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi na kuiomba Tarura kuangalia uwezekano wa kuruhusu watembea wa miguu wakati wakiendelea kukamilisha ujenzi huo.

“Daraja hili tumelipambania na mheshimiwa diwani na wajumbe ambao walikuwa wanapaza sauti zao, niwashukuru watu wa Tarura ujenzi unakwenda haraka,” amesema Bonnah.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.