Wanafunzi kutoka mikoa mitano Bara na Visiwani kutembelea Makumbusho ya Taifa Julai 5

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital Wanafunzi kutoka mikoa mitano ya Bara na Visiwani wanatarajia kutembelea Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) mnamo Julai 5, 2024, ili kupata ujuzi zaidi kwa vitendo. Hayo yamebainishwa leo Julai 1, 2024, na Afisa Utamaduni wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Chance Ezekiel, wakati […]

Jul 2, 2024 - 19:00
 0
Wanafunzi kutoka mikoa mitano Bara na Visiwani kutembelea Makumbusho ya Taifa Julai 5

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Wanafunzi kutoka mikoa mitano ya Bara na Visiwani wanatarajia kutembelea Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) mnamo Julai 5, 2024, ili kupata ujuzi zaidi kwa vitendo.

Hayo yamebainishwa leo Julai 1, 2024, na Afisa Utamaduni wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Chance Ezekiel, wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Utalii, Nkoba Mabula, alipotembelea banda lao lililopo kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba.

Ezekiel amesema wanafunzi kutoka Zanzibar wanaotarajiwa kufika hadi sasa ni 22, huku Bara wanafunzi 12 wakiendelea kujisajili na idadi yao inatarajiwa kuongezeka kadri siku zinavyosogea. “Wanafunzi watakiwa kujifunza vitu mbalimbali kwa vitendo kwa sababu shuleni wanasoma kwa nadharia. Wanatakiwa kutembelea Makumbusho ya Taifa mbalimbali ili waone kwa uhalisia na kujifunza,” amesema Ezekiel.

Ameongeza kuwa wana urithi usio shikika wa uchanja chale na ndonya wa kabila la Makonde umehifadhiwa kidigitali, na kutoa nafasi kwa mtazamaji kupiga picha kupitia mitandao ya kijamii na kufurahia na marafiki zake kwa teknolojia ya “Augmented Reality” (AR).

Ezekiel pia ameongeza kuwa wanafungua fursa za uwekezaji na biashara kwa Watanzania kwenye maeneo ya mali kale na makumbusho, ikiwemo biashara ya vyakula na huduma mbalimbali kwa watalii pamoja na ujasiriamali wa bidhaa za kiutamaduni na asili ya Mtanzania. Aidha, amesema wanakuza utalii wa matasha ya Utamaduni kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.