Wizara ya Ulinzi yajivunia mafanikio miaka 60 ya Muungano

Na Ramadhan Hassan,Dodoma WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, imetaja mafanikio iliyopata kuelekea miaka 60 ya Muungano,huku ikisema takwimu zinaonesha zaidi ya asilimia 80 ya wananchi raia wasiyo wanajeshi wanapata huduma za afya katika hospitali za Jeshi. Mafanikio hayo yametajwa leo April 3,2024 Jijini hapa na Waziri wa Wizara hiyo,Dk Stergomena Tax wakati […]

Apr 3, 2024 - 13:00
 0
Wizara ya Ulinzi yajivunia mafanikio miaka 60 ya Muungano

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, imetaja mafanikio iliyopata kuelekea miaka 60 ya Muungano,huku ikisema takwimu zinaonesha zaidi ya asilimia 80 ya wananchi raia wasiyo wanajeshi wanapata huduma za afya katika hospitali za Jeshi.

Mafanikio hayo yametajwa leo April 3,2024 Jijini hapa na Waziri wa Wizara hiyo,Dk Stergomena Tax wakati akileza mafanikio ya miaka 60 ya Muungano kwa Waandishi wa Habari.

Waziri Stergomena amesema wanapoazimisha miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, inayo kila sababu ya kujivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika awamu zote sita za uongozi.

Amesema kwenye sekta ya afya wizara imefanikia katika utoaji wa huduma za afya na tiba kupitia hospitali za Jeshi.

Amezitaja hospitali hizo kuwa ni Lugalo Dar es Salaam, MH Mwanza, Bububu Zanzibar, Mirambo Tabora, MH Arusha, MH Mbeya ambazo hutoa huduma kwa wanajeshi, wananchi waishio maeneo yaliyo jirani na kambi za jeshi na katika hospitali nyingine.

“Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wanaopata huduma katika hospitali za Jeshi ni raia wasiyo wanajeshi,”amesema Waziri Stergomena.

Amesema katika kulinda mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uhuru, na usalama wa nchi, wizara kupitia JWTZ imechangia katika kujenga uchumi imara ambapo wananchi hujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali bila hofu.

Aidha, Serikali kupitia Wizara imeendelea kutekeleza, na kuliimarisha Jeshi kwa kulipatia zana na vifaa bora na vya kisasa, rasilimali watu, na nyenzo za kufanyia mazoezi ili kuwa imara wakati wote.

“Ili kuliimarisha Jeshi, Serikali kupitia Wizara imeendelea kuboresha maslahi kwa Wanajeshi na Watumishi wa Umma kadri uwezo wa kifedha unavyoruhusu, kwa kuwapatia makazi bora kwa kuwajengea nyumba, pamoja na stahili mbalimbali, kupandisha vyeo kulingana na sifa, vigezo na taratibu,”amesema Waziri Stergomena.

Waziri huyo amesema hadi sasa Serikali imejenga nyumba za makazi katika kambi mbalimbali za Jeshi kwenye mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kagera, Kigoma, Morogoro, Mwanza, Pemba, Pwani, Rukwa, Tabora, na Tanga.

Aidha, ujenzi wa nyumba hizo, kwa kiasi kikubwa umepunguza uhaba wa nyumba pamoja na changamoto zitokanazo na wanajeshi kuishi uraiani.

Ameutaja mchango mwingine mkubwa wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania katika miaka 60 ya Muungano, ni ulinzi madhubuti wa mipaka yetu, uhuru, na katiba.

Amesema nchi imeendelea kuwa imara na yenye amani katika awamu zote.

Mafanikio mengine ni ushiriki wa Wizara kupitia Taasisi zake, hususan JWTZ katika kukabiliana na majanga au maafa mbalimbali pale yanapotokea.

Amesema katika kutekeleza jukumu hilo, JWTZ imeendelea kushiriki kikamilifu katika kutoa misaada ya uokoaji na ile ya kibinadamu kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

Pia amesema Wizara kupitia JWTZ imeendelea kushirikiana na mamlaka za kiraia katika miradi ya kimkakati.

“Baadhi ya maeneo ambayo JWTZ imeshirikiana na mamlaka za kiraia ni pamoja na kushiriki katika kuboresha huduma katika taasisi za serikali; kushiriki katika ulinzi wa miradi na maeneo ya kimkakati kwa nchi ikiwemo katika migodi mbalimbali.

“Ulinzi wa miundombinu kama reli, ikiwa ni pamoja na reli ya kisasa Standard Gauge Railway (SGR), Mradi wa Bwawa la kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (Julius Nyerere Hydro Power Project – JNHPP); ulinzi katika mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA), kampuni ya simu (TTCL), na maeneo ya viwanja vya ndege,”amesema Waziri Stergomena

Ameyataja mafanikio mengine ni kutungwa kwa Sheria ya JKT Na. 16 ya mwaka 1964 (The National Service Act No. 16 of 1964) ambayo iliwezesha kuanzishwa kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

“Sheria hiyo imefanyiwa marekebisho mbalimbali hadi mabadiliko ya mwaka 2002. Sheria hiyo imewezesha kuandikishwa vijana wa kujitolea, na kwa mujibu wa sheria,”amesema Waziri huyo.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.