Yanga yalamba mkataba mnono

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital KLABU ya Yanga imeingia mkataba na Shirika la Bima la Taifa (NIC) wa kudhamini tuzo za mchezaji bora wa mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu wenye thamani ya shilingi milioni 900. Akizungumzia mkataba huo leo Oktoba 9,2023 mbele ya waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, Rais wa  klabu hiyo, […]

Oct 9, 2023 - 14:00
 0
Yanga yalamba mkataba mnono

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

KLABU ya Yanga imeingia mkataba na Shirika la Bima la Taifa (NIC) wa kudhamini tuzo za mchezaji bora wa mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu wenye thamani ya shilingi milioni 900.

Akizungumzia mkataba huo leo Oktoba 9,2023 mbele ya waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, Rais wa  klabu hiyo, Mhandishi Hersi Said, amesema ni heshima kubwa waliyopewa na shirika hilo na makubaliano  hayo yatanufaisha pande zote mbili  kibiashara.

Rais huyo wa timu ya Wananchi, ameeleza kuwa kilichochangia kupata udhamini ni kutokana na uwepo wa wachezaji wenye ubora katika kikosi chao ambao wana ushawishi mkubwa  ndani na nje ya uwanja.

“Tunaelewa kwa nini NIC wamechagua kufanya kazi na sisi, ni kwa sababu tuna wachezaji bora zaidi ambao huwezi kuwapata kwenye klabu nyingine. Wachezaji hawa wana ushawishi mkubwa nje na ndani ya uwanja. Ushawishi wao ni chachu ya kutangaza biashara hii ya Bima,” amesema Hersi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Elirehema Doriye, ameeleza kuwa wamefanya hivyo ili kuwapa wachezaji motisha na mashabiki sehemu ya kuzungumzia kwa kuchagua mchezaji wao bora.

“Utaratibu utakaotumika kumpata mchezaji bora wa mwezi ni jobo la benchi la ufundi kuchagua  wachezaji watatu, kasha mashabiki watampigia kura mmoja,” amesema Doriye.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.