Zanzibar yaanza vibaya CECAFA

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital TIMU ya soka ya wasichana ya Zanzibar wenye umri chini ya miaka 18, imeanza vibaya mashindano ya CECAFA kwa kufungwa na Uganda mabao 3 -0 katika mchezo uliopigwa leo Julai 27, 2023 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Mabao yote ya Uganda yalifungwa kipindi cha pili Patricia Nanyazi, […]

Jul 27, 2023 - 17:00
 0
Zanzibar yaanza vibaya CECAFA

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

TIMU ya soka ya wasichana ya Zanzibar wenye umri chini ya miaka 18, imeanza vibaya mashindano ya CECAFA kwa kufungwa na Uganda mabao 3 -0 katika mchezo uliopigwa leo Julai 27, 2023 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mabao yote ya Uganda yalifungwa kipindi cha pili Patricia Nanyazi, Agnes Nabukenya, Phionah Nabulime.

Akizungumzia matokeo hayo, kocha wa Zanzibar, Abdulmutik Haji, amesema kipindi cha kwanza walianza vizuri na kwenda mapumziko bila kuruhusu bao.

Alieleza kuwa pamoja na timu yake kucheza vizuri lakini kipindi cha pili walishindwa kupiga pasi za mwisho kutokana na kudhibitiwa na wapinzani.

Amesema tatizo hilo ameliona na anakwenda kulifanyia kazi kabla ya kukutana na Tanzania Bara, Julai 30, 2023.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.