Demokrasia iendane na mazingira-Balozi Battle

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital BALOZI wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle, amesema demokrasia ya nchi inapaswa kuendana na mazingira yake mahususi badala ya kutegemea kufanana duniani. Akizungumza katika Mkutano wa Demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Balozi Battle amasema kwa mfano demokrasia ya Tanzania haiwezi kufanana na demokrasia ya nchi za kifalme […]

Aug 23, 2023 - 14:00
 0
Demokrasia iendane na mazingira-Balozi Battle

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

BALOZI wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle, amesema demokrasia ya nchi inapaswa kuendana na mazingira yake mahususi badala ya kutegemea kufanana duniani.

Akizungumza katika Mkutano wa Demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Balozi Battle amasema kwa mfano demokrasia ya Tanzania haiwezi kufanana na demokrasia ya nchi za kifalme (kama Uingereza) na sio lazima ifafane na mifumo mingine ya kiutawala inayotumiwa na nchi nyingine duniani.

“Demokrasa ya Tanzania ni lazima izingatie muktadha na mazingira ya Tanzania, na iakisi matakwa ya watazania wenyewe. Nchi yotote duniani haina haki ya kuipangia Tanzania aina ya mfumo wake wa demokrasia,” alisema Balozi Battle.

Aidha, Balozi Battle amesema Marekani inajivunia sana hatua kubwa alizochukua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuboresha demokrasia nchini Tanzania.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.