Kituo cha Afya Gumanga chafanya upasuaji mkubwa wa kwanza

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Kituo cha Afya cha Gumanga kilichopo kata ya Gumanga Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kimefanikiwa kufanya upasuajia mkubwa wa kwanza wa dharura kwa mama mjamzito toka kufunguliwa kwake. Akizungumza mara baada ya upasuaji huo, Mganga Mkuu wilaya ya Mkalama, Dk. Solomon Michael amesema upasuaji huo umefanyika Julai 01,2024 chini ya […]

Jul 3, 2024 - 01:00
 0
Kituo cha Afya Gumanga chafanya upasuaji mkubwa wa kwanza

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kituo cha Afya cha Gumanga kilichopo kata ya Gumanga Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kimefanikiwa kufanya upasuajia mkubwa wa kwanza wa dharura kwa mama mjamzito toka kufunguliwa kwake.

Akizungumza mara baada ya upasuaji huo, Mganga Mkuu wilaya ya Mkalama, Dk. Solomon Michael amesema upasuaji huo umefanyika Julai 01,2024 chini ya madaktari wawili wakisaidiwa na wauguzi pamoja na mtalaamu wa uzingizi.

“Kwa mara ya kwanza tumefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa hapa Gumanga toka tuanzishe huduma hizi za upasuaji. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu.Mtoto aliyezaliwa ni wakike na uzito wa kilo 3.1, hali ya mama na mtoto inaendelea vizuri,” aliongeza Dk. Michael.

Kwa mujibu wa Dk. Solomon Michael amesema mjamzito huyo amefika kituoni hapo siku ya Jumatatu ya Julai 1,2024 muda wa asubuhi na kufanyiwa upasuaji muda wa saa moja usiku.

Dk. Sira Laurent Kisamhara, akisaidiwa na Dk. Lazaro Chambo, wauguzi wakiwa Seleman Mwalukasa, Faraja Shadrack, na Richard Sopeter mtaalamu wa usingzi pamoja a mtaalam wa Maabara, Patric Sanga.

Kituo cha afya cha Gumanga kinakuwa ni kituo cha tatu cha serikali wilayani Mkalama kinachotoa huduma za upasuaji, vingine ni Hosipitali ya Wilaya ya Mkalama pamoja na kituo cha Afya cha Kinyambuli.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.