MwanaFA azindua ofisi za Yanga

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’, leo Februari 7, 2024 ameshiriki uzinduzi wa ofisi za Klabu ya Yanga zilizopo Jangwani Dar es Salaam baada ya kufanyiwa maboresho. Akizungumza katika uzinduzi huo, ameupongeza uongozi wa Yanga kwa kitu walichofanya kwani kutokana na jengo hilo ni […]

Feb 7, 2024 - 12:00
 0
MwanaFA azindua ofisi za Yanga

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’, leo Februari 7, 2024 ameshiriki uzinduzi wa ofisi za Klabu ya Yanga zilizopo Jangwani Dar es Salaam baada ya kufanyiwa maboresho.

Akizungumza katika uzinduzi huo, ameupongeza uongozi wa Yanga kwa kitu walichofanya kwani kutokana na jengo hilo ni la zamani imekuwa ngumu kuamini kama kuna shughuli za ukarabati zinafanyika, akijua wameshakata tamaa.

“Nimekuwa nikipita hapa Jangwani sijawahi kufahamu kama kuna shughuli zinaendelea humu ndani. Lakini kwa hili ambalo mmelifanya, kweli ni ishara thabiti ya namna klabu kubwa inavyofanya mambo yake. Nilidhani Injinia Hersi umekata tamaa lakink kumbe ulikuwa na mpango mkubwa,” amesema Naibu waziri huyo.

Amesema uboreshaji huo wa jengo hilo, ni maendeleo ambayo klabh kubwa kama Yanga inatakiwa kufanya.

Ameeleza kuwa uwepo wa jengo hilo lililojengwa miaka 53 ni maono ya wazee wa zamani akiwamo Hayati Abeid Amani Karume ambaye alifikiria na kuweka nguvu zake na hadi leo jengo linaweza kuhudumia klabu ya mwaka 2024.

Kwa upande wake Rais wa Yanga, Injinia Hersi ameweka wazi kuwa ofisi hizo zimefanyiwa ukarabati kwa miaka mitatu ambalo walikuwa wamepata hifadhi kwenye jengo la mdhamini wao Ghalib Said.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.