Rai yatolewa kwa wakopaji fedha

Na Mwandishi Wetu, Morogoro Wananchi wametakiwa kukopa kwenye taasisi za fedha zilizosajiliwa na kutambulika na Benki Kuu ya Tanzania au Mamlaka Kasimishwa ili kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza kwa mkopaji. Rai hiyo imetolewa mkoani Morogoro na Ofisa Msimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha,  Salim  Kimaro, wakati akifungua […]

Jan 16, 2024 - 06:00
 0
Rai yatolewa kwa wakopaji fedha

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Wananchi wametakiwa kukopa kwenye taasisi za fedha zilizosajiliwa na kutambulika na Benki Kuu ya Tanzania au Mamlaka Kasimishwa ili kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza kwa mkopaji.

Rai hiyo imetolewa mkoani Morogoro na Ofisa Msimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha,  Salim  Kimaro, wakati akifungua mafunzo ya elimu ya fedha kwa wasanii kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI).

Amesema kuwa mkopaji anapaswa kuwa na elimu sahihi kuhusu huduma za fedha
na kusoma na kuelewa vyema mikataba ya mikopo ili kufahamu gharama halisi za mkopo na kuziafiki kabla ya kuchukua  ili kuepuka kuingia hasara kwa kudhulumiwa.

“Mpango mkuu wa maendeleo ya sekta ya fedha, umeelekeza kutoa elimu ya fedha kwa umma kwa njia mbalimbali, hivyo mafunzo kwa wasanii yatawezesha kupeleka elimu ya fedha vijijini ambako kumekuwa na uelewa mdogo wa masuala hayo na kusababisha uwepo na mikopo umiza,” amesema Kimaro.

Amesema kuwa mwananchi anapokopa ni lazima ajue riba, ada na gharama zingine lakini pia mkopaji anapaswa kujua kiasi ambacho anatakiwa kulipa kwa kipindi chote cha mkopo.

Kimaro, amesema kuwa programu ya elimu kwa umma inatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitani kuanzia 2020/2021 hadi 2025/2026 ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa miaka 10 kuanzia 2020/2021hadi 2029/2030.

Ameeleza kuwa baada ya hapo mpango mkuu utafanyiwa tathmini ili kuona mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wake na kuja na maboresho iwapo changamoto zitajitokeza.

Amesema kuwa sanaa ni eneo muhimu la kufikisha ujumbe kwa umma kwa kuwa ni rahisi kuwafikia wananchi na njia yenye mafanikio makubwa si tu kwa Tanzania lakini pia duniani kwa ujumla.

Amebainisha kuwa maeneo muhimu ambayo yataangaziwa wakati wa kutoa elimu ya fedha ni pamoja na usimamizi wa fedha binafsi, uwekaji wa akiba, mikopo, uwekezaji, bima, bima ya amana, mpango wa kujiandaa na maisha ya uzeeni, kodi, mifumo ya malipo na kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha.

“Tutaenda vijijini na tutachagua maeneo ambayo elimu ya fedha ipo chini baada ya wasanii kupata uelewa ili kupeleka elimu sahihi kwa wananchi,” ameongeza.

Aidha amesema kuwa mkopaji anashauriwa kukopa kwa ajili ya uwekezaji unaozalisha kama vile kununua sehemu ya ardhi ambapo ataweza kuzalisha mazao au kupanua biashara itakayomwezesha mkopaji kurejesha mkopo kwa wakati na kuweza kukopa zaidi baadae kama atahitaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI), Aline Augustin, amesema kuwa upekee katika kuelimisha jamii ni matumizi ya sanaa za maonesho jukwaani kwa ajili ya maendeleo ya jamii, kwa kutumia pia ngoma bila maneno na maigizo kwa njia ya redio.

“Kwa njia ya redio na ngoma TACCI, inakuwa na nafasi kubwa ya kuifikia jamii na kupenyeza elimu na kuvutia watu wa makundi tofauti kwa kuwaleta pamoja na kuchochea mazungumzo na majadiliano katika elimu inayotolewa,’’ amesema Augustin.

Aidha amesema kuwa mafunzo ya elimu ya fedha yanayoendelea kutolewa yanawapa uelewa na wigo mpana wa kuandaa elimu kwa njia ya sanaa itakayokidhi matakwa ya Wizara ya Fedha katika kufikisha ujumbe stahiki kwa wananchi hususani waishio vijijini.

Augustine, ameipongeza Wizara ya Fedha kwa kuamua kutumia sanaa kufikisha elimu vijijini na ameahidi kutumia mafunzo wanayopata kuongeza ujuzi na kuhakikisha elimu ya fedha kwa njia ya sanaa inawasilishwa kwa ufanisi na kwa tija.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.