TCCIA kuimarisha ushirikiano Sekta binafsi, Serikali

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital Rais wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA), Vicent Minja, amesema uongozi mpya umeweka mikakati ya kuhakikisha sekta binafsi inashirikiana na Serikali katika kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 10,2023, jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kodi mpya, Minja amesema TCCIA imejipanga kuhakikisha […]

Nov 11, 2023 - 12:00
 0
TCCIA kuimarisha ushirikiano Sekta binafsi, Serikali

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

Rais wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA), Vicent Minja, amesema uongozi mpya umeweka mikakati ya kuhakikisha sekta binafsi inashirikiana na Serikali katika kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 10,2023, jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kodi mpya, Minja amesema TCCIA imejipanga kuhakikisha inaimarisha ushirikiano wa dhati na wanachama,wafanyabiashara na wadau ili kuhakikisha sauti zao zinasikika.

“Tutaendelea kushirikiana kwa karibu na serikali na wadau wengine ili kuhakikisha biashara,viwanda na kilimo vinapiga hatua na tunaweka mikakati imara ya kuvutia uwekezaji,kutoa mafunzo na kusaidia miradi inayochangia ukuaji wa sekta hizi”amesema Minja.

Ameongeza kuwa wataendeleza ubunifu na teknolojia katika utoaji wa vyeti vya uasili ambapo wanahimiza matumizi ya teknolojia na ubunifu katika biashara,viwanda na kilimo.

Amesema uongozi huo umejipanga kuimarisha ushirikiano na serikali,taasisi ,balozi, wadau wa maendeleo na chemba za kimataifa lengo kufikia maendeleo endelevu.

Amesema kwa kutumia uzoefu wao wa miaka 35 katika huduma na uongozi wa sekta binafsi nchini wataendelea kusimamia mabalaza ya biashara.

Naye Makamu wa Rais wa Kilimo TCCIA, Swallah Swallah, amesema zaidi ya asilimia 90 ya watanzania wapo katika sekta ya kilimo, hivyo wamejipanga kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kuwa mhimili wa uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Biashara TCCIA, Boniface Ndego, amesema wamejipanga kuchochea mageuzi makubwa kwenye masoko ili kujenga uchumi wa taifa.

Aidha ameongeza kuwa wataunganisha sekta binafsi na kuchochea ujenzi wa kampuni kubwa ili kutanua wigo wa biashara lakini pia kuwezesha mitaji ya kuanzisha biashara mpya na kuendeleza biashara.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.