Wafanyabiashara Tanzania, Indonesia wakutana

Na Mwandishi wetu, Jakarta Indonesia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu na kushiriki kwenye Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Indonesia lililofanyika Januari 25, 2024 katika jiji la Jakarta. Kongamano hilo ni sehemu ya ziara ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ilioanza Januari, 24 2024 yenye lengo la kuendeleza na […]

Jan 26, 2024 - 12:00
 0
Wafanyabiashara Tanzania, Indonesia wakutana

Na Mwandishi wetu, Jakarta Indonesia

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu na kushiriki kwenye Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Indonesia lililofanyika Januari 25, 2024 katika jiji la Jakarta.

Kongamano hilo ni sehemu ya ziara ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ilioanza Januari, 24 2024 yenye lengo la kuendeleza na kukuza mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi hizi na hasa kuhamasisha biashara na uwekezaji kwa pande zote mbili.

Taasisi mbalimbali za sekta binafsi na umma pamoja na wafanyabiashara kutoka Tanzania wamekutana na wenzao wa Indonesia kubadilishana fursa baina yao.

Katika kongamano hilo Rais Dk.Samia amewahakikishia wafanyabiashara wa Indonesia na Tanzania mazingira mazuri yatakayoendelea kukuza biashara baina ya nchi hizi mbili ikiwa ni pamoja na sera thabiti za kisiasa na uchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa Mohamed Khamis pamoja na Soegeng Hernowo, Mkurugenzi Mkuu wa PT PPI walisaini na kubadilishana hati ya makubaliano ya ushirikiano katika ukuzaji biashara kwa nchi zote mbili.

Mkurugenzi wa TanTrade pia alitumia fursa hiyo kuainisha fursa za biashara zilizopo Tanzania na kueleza kuwa TanTrade itaendelea kuibua fursa kwa wadau wa biashara nchini na kuratibu mikutano ya biashara na kuhakikisha wafanyabiashara wa Tanzania wanaunganishwa na wafanyabiashara wa Indonesia ili kupata soko la bidhaa zinazozalishwa nchini.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.