TRA yapongeza juhudu za wadau

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata amepongeza juhudi zinazofanywa na forodha na wadau katika ukusanyaji wa kodi nchini. Hayo ameyasema leo Januari 26,2024 jijini Dar es Salaam na wakati wa utaoaji wa vyeti vya siga, ikiwa ni maadhimisho ya siku ya forodha duniani ambayo kufanyika Januari 26 […]

Jan 26, 2024 - 12:00
 0
TRA yapongeza juhudu za wadau

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata amepongeza juhudi zinazofanywa na forodha na wadau katika ukusanyaji wa kodi nchini.

Hayo ameyasema leo Januari 26,2024 jijini Dar es Salaam na wakati wa utaoaji wa vyeti vya siga, ikiwa ni maadhimisho ya siku ya forodha duniani ambayo kufanyika Januari 26 kila mwaka.

Amesema maadhimisho hayo yalianzishwa tangu mwaka 1964 kwa lengo la kutoa vyeti vya sifa kwa wadau wa forodha.

Naye Kaimu Kamishna wa Forodha wa TRA, Juma Hassan amesema maadhimisho hayo ni kudhihirisha kwa umma kazi zinazofanywa na forodha kwa kushirikiana na wadau.

Amesema jukumu la msingi la forodha ni kurahisisha biashara lakini kutekeleza majukumu kuhakikisha watu wanalipa kodi kabla ya kuingiza mzigo.

“Kuwatambua wadau wote na kazi tunazofanya, kuwatambua washirika wa zamani na wapya na taasisi kutoa miongozo ya bidhaa zinazoingia nchini,”amesema Hassan.

Ameeleza kuwa wao kama forodha jukumu lao ni kukagua mzigo kushirikiana na taasisi zote zinazofanya kazi kwa pamoja hivyo wameanzisha mfumo wa ‘single window’ na taasisi zote zinafanyaka kazi kwa mfumo huo mmoja kuondoa vikwazo kwa walipa kodi.

Aidha amesema wameongeza k ushirikiano kwa sababu forodha yenyewe haiwezi kutimiza majukumu hayo bila kushirikiana na Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) na taasisi zinazohusika.

“Kuendelea kuboresha mifumo na kuongeza ufanisi, ubunifu katika kazi zetu kwa weledi,” amesema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema uchumi wa Tanzania unakua kupitia forodha kwa kusimamia sheria za forodha duniani na nchini.

Ametoa wito kwa wadau kuendelea kulipa kodi stahiki na kuhakikisha hawakwepi kodi na kuwa wazalendo katika nchi yao.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maaluumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema ni siku muhimu ya forodha duniani kwa mfanyabiashara mdogo, kati na mkubwa.

Amesema wataendelea kuimarisha usalama maeneo mbalimbali kwa kuwa ni wajibu wao kama Jeshi la Polisi.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.