Wakazi wa kijiji cha Kondo waonywa kuharibu misitu ya mikoko

Na Upendo Mosha, Bagamoyo WAKAZI wa kijiji Kondo, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani wameonywa kuacha tabia ya kuharibu Mistu ya mikoko iliyopo pembezoni mwa habari ya Hindi, ili kuthibiti tatizo la kuharibu wa mazingira na mazalia ya samaki. Rai hiyo ilitolewa Jana na Mkurugenzi wa uratibu na ufuatiliaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini(TASAF), Haika […]

Jun 27, 2024 - 22:00
 0
Wakazi wa kijiji cha Kondo waonywa kuharibu misitu ya mikoko

Na Upendo Mosha, Bagamoyo

WAKAZI wa kijiji Kondo, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani wameonywa kuacha tabia ya kuharibu Mistu ya mikoko iliyopo pembezoni mwa habari ya Hindi, ili kuthibiti tatizo la kuharibu wa mazingira na mazalia ya samaki.

Rai hiyo ilitolewa Jana na Mkurugenzi wa uratibu na ufuatiliaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini(TASAF), Haika Shayo,.wakatii wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya mfuko huo, inayotekelezwa wilaya huo, ambapo aliongozana na wadau wa maendeleo (wafadhili).

Alisema tatizo la uharibufu wa mikoko katika eneo hilo unaathari kubwa kwa wananchi wa kijiji hicho ambao shughuli zao za uchumi zinategemea uvuvi na kwamba hatua za kudhibiti hali hiyo zinapaswa kuchukuliwa.

“Tabia ya ukataji wa miti aina ya mikoko kando kando ya bahari imekuwa haijengi bali inabomo na waathirika wakubwa ni sisi wenyewe, hivyo ni vema mkaacha na mkatunza mikoko”alisema.

Mbali na hilo kuhusu Mkurugenzi huyo amepongeza juhudi ambazo zimeanza kuchukuliwa na wanufaika wa mfuko huo kwa kupanda mikoko zaidi ya 200,000 katika eneo lenye ukubwa wa hekari 12.

Alisema hatua hiyo ni ya kuigwa na kupongezwa kwani imeanza kurejesha uoto wa asili ambao ulikuwa umeharibiwa na kuanza kutoweka.

“Niwapokeze kwa hatua hii na wenyewe mmekiri baadhi ya samaki adimu kama Kaa wameanza kurejea baada ya mikoko hii kupandwa …Kwa maana nyingine wananchi mtaendaj kunufaika moja Kwa moja na uchumi wa Buluu ambao serikali imekuwa ikiuimoza kwenye,” alisema.

Aidha aliwataka wakazi hao kuendelea juhudi hizo Kwa kupanda mikoko katika maeneo yalioathirika ili kuunga mikono juhudi za serikali za kufanya Tanzania kuwa nchi ya kijana na kuimarisha uchumi wa buluu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho, Jafary Athuman, alisema wananchi walichukua hatua hiyo baada ya kuona adhari za moja Kwa moja za uharibufu wa mazingira ambao umeanza kukikumba kijiji hicho ikiwemo mazalia ya samaki kutoweka na kuongezeka kwa kina cha maji.

Naye mwananchi wa kijiji hicho Mwanaheri Maulid, amishukuru TASAF, ambaye aliingozwa katika mpango huo 2014, ameupongeza mfuko huo kwa ruzuku wanazotoa Kwa walengwa ambapo Kwa upande wake ameweza kusomesha watoto wake na kufanya shughuli nyingine za uchumi.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.