Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali watu waaswa kushirikiana na OSHA kulinda nguvu kazi

N Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umewataka Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali watu kushirikiana na taasisi hiyo katika kuimarisha mifumo ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya katika maeneo yao ya kazi ili kuleta tija kwa taifa. OSHA imetoa wito huo jana kupitia kwa […]

Oct 13, 2023 - 21:00
 0
Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali watu waaswa kushirikiana na OSHA kulinda nguvu kazi

N Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umewataka Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali watu kushirikiana na taasisi hiyo katika kuimarisha mifumo ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya katika maeneo yao ya kazi ili kuleta tija kwa taifa.

Mkaguzi wa Afya wa OSHA, Dk. Edwin Senguo akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma kuhusu masuala mbalimbali ya usalama na afya mahali pa kazi mara baada ya OSHA kuwasilisha mada katika kikao hicho.

OSHA imetoa wito huo jana kupitia kwa Afisa Mafunzo wake, Simon Lwaho mara baada ya kuwasilisha mada ya masuala ya usalama na afya mahali pa kazi ulioenda sambamba na zoezi la upimaji wa magonjwa yatokanayo na kazi katika Kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma kinachofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC).

“Kupitia kikao kazi hiki tumewaeleza Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali watu kuwa wanapowekeza katika kulinda usalama na afya za wafanyakazi wao wanaongeza tija katika utoaji wa huduma katika maeneo yao ya kazi, taasisi ya OSHA inaendelea kuwakumbusha wakuu hawa kuhakikisha wanashirikiana nasi katika kuimarisha mifumo ya usalama na afya mahali pa kazi kwasababu ni hitaji la kisheria linalotakiwa kusimamiwa kwa kuhusisha wadau wakubwa watatu ambao ni sisi OSHA kwa upande wa serikali, wao Wakuu wa Idara za Utawala pamoja na wafanyakazi ambao ni kiungo muhimu katika kuleta maendeleo ya taifa letu,” alisema Simon Lwaho.

Mkaguzi wa Afya wa OSHA,  Amina Nangu akimpima macho mdau kwa kutumia mashine ya kisasa ya VT 1 katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma Mkoani Arusha.

Aidha Mkaguzi wa Afya wa OSHA, Amina Nangu amesema kuwa Wakuu hawa wa Idara za Utawala ndio watoa maamuzi katika maeneo yao ya kazi hivyo wakielewa vyema Sheria na miongozo ya usalama na afya mahali pa kazi wataweza kuisimamia utekelezaji wake ipasavyo.

“OSHA tumeshiriki katika kikao kazi hiki ili kutoa elimu kadhalika kuendesha zoezi la upimaji wa magonjwa yatokanayo na kazi tukiamini kuwa wakuu hawa wa idara za utawala wakielewa vizuri umuhimu wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi basi wataweza kusimamia na kuteleleza vizuri sheria na miongozi hii kwasababu wao ndio watoa maamuzi katika maeneo yao ya kazi,” alisema Amina.

Kwa upande wao wakuu hao wa Idara za Utawala katika Utumishi wa Umma kutoka maeneo mbalimbali nchini wamekiri kuwa ni muhimu sana watumishi kutambua hali zao za kiafya hususan kufanya uchunguzi wa magonjwa yatokanayo na kazi huku wakiahidi kuitumia vyema elimu iliyotolewa na OSHA kupitia kikao kazi hicho.

“Ni muhimu sana kwa watumishi wa umma kufanya uchunguzi wa magonjwa yatokanayo na kazi kwa sabababu hii itasaidia kutambua hali zetu za kiafya ikiwemo kubaini kama kuna madhara yoyote yaliyotokana na kazi tunazofanya pia elimu hii iliyotolewa na OSHA itatusaidia katika kuepukana na vihatarishi mbalimbali vya ajali na magonjwa katika maeneo yetu ya kazi,” alisema Judith Bosco.

Naye, Erick Bazompora ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala katika Manispaa ya Bukoba amesema kuwa watumishi wanapotambua hali zao za kiafya mapema ni rahisi kujikinga dhidi ya madhara husika na kwa kufanya hivyo itasaida kupunguza gharama za uendeshaji wa eneo la kazi pamoja na kuleta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla kutoka na kuwa wafanyakazi hawa wanafanyakazi katika mazingira salama na yanayolinda afya zao.

Kikao Kazi hicho cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma kinafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 11 hadi 13, 2023 na kilifunguliwa rasmi na Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene kikiongozwa na kauli mbiu inayosema: “Usimamizi wa Rasilimali Watu Unaozingatia Maadili, Sheria, Uwajibikaji na Matumizi ya TEHAMA ni Msingi wa Utaoaji Huduma Bora katika Sekta ya Umma”

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.