Watendaji Wizara ya Madini watakiwa kupanga mikakati kuongeza Bajeti ya Wizara

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amewataka Watendaji wa Wizara na Taasisi  kujipanga  kimkakati kwa kubuni  miradi yenye tija kwenye Sekta ya Madini itakayowezesha  kuongeza Bajeti ya Wizara  na  kuhakikisha inakwenda  sambamba na Vipaumbele vya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, Dira ya 2030 Madini ni Maisha na Utajiri […]

Oct 7, 2023 - 13:00
 0
Watendaji Wizara ya Madini watakiwa kupanga mikakati kuongeza Bajeti ya Wizara

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amewataka Watendaji wa Wizara na Taasisi  kujipanga  kimkakati kwa kubuni  miradi yenye tija kwenye Sekta ya Madini itakayowezesha  kuongeza Bajeti ya Wizara  na  kuhakikisha inakwenda  sambamba na Vipaumbele vya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, Dira ya 2030 Madini ni Maisha na Utajiri pamoja na Vipaumbele vya Taifa.

Ametoa rai hiyo leo Oktoba 6, 2023, wakati wa kikao chake na baadhi ya Watendaji hao wa Wizara na Wakuu wa Taasisi za Wizara, ambacho pia kimehusisha watendaji wanaohusika na masuala ya Mipango, Fedha na Rasilimaliwatu kilicholenga kujadili na kujipanga kutekeleza maelekezo, vipaumbele vya Wizara, majukumu, mipango na program mbalimbali ambazo zilijadiliwa wakati wa vikao vya Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alivyofanya na taasisi zote chini ya Wizara baada ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Waziri wa Madini kwa lengo la kufahamiana, kujengeana uelewa na kuweka mikakati ili kuongeza tija kwenye Sekta ya Madini.

Aidha, katika kikao hicho, watendaji hao wamepata wasaa wa  kufahamishwa kuhusu namna  ya kuandaa mipango na miradi ya kisekta yenye  tija kwa taifa  kwa kuhakikisha inakwenda sambamba na vipaumbele vilivyopangwa na Wizara na vile vya kitaifa.

Akizungumza katika kikao hicho, Mchumi Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango, Khalid Shekimweli amesisitiza kuwa miradi na mipango inayopangwa na sekta ni vema ikazingatia maeneo makuu ya msingi ambayo ni pamoja na kuzingatia masuala yanayohusu huduma muhimu za kijamii, yanayokusudia kuondoa umaskini pamoja na kukuza uchumi.

Awali, Mkurugenzi wa Sera na Mipango  Wizara ya Madini, Augustino Olal ameeleza kuwa katika Mwaka wa Fedha wizara imepangiwa bajeti ya Sh bilioni 89.3 ambayo imelenga kutekeleza vipaumbele Sita vya Wizara na kuvitaja kuwa ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli, kuongeza Mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa;  kuendeleza Madini Muhimu na Madini Mkakati; Kuwaendeleza na kusogezaHuduma za Ugani kwa Wachimbaji wadogo; kuhamasisha shughuli za Uongezaji thamani Madini na kuhamasisha uwekezaji na Biashara katika sekta ya Madini na Uanzishwaji wa Minada na Maoneshi ya Madini ya Vito.
If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.