Lavauda awapa shavu Tiwa Savage, Kanis, Reekado Banks&Patoranking kwenye Roll on Me

Na Joseph Shaluwa STAA wa kike kwenye uwezo mkubwa katika kuimba na kutunga, Lavaud amerejea kwa kishindo baada ya kuachia singo kali inayokwenda kwa jina la “Roll on Me” – ikiwa kwenye mitandao ya Saint & Citizen Music. Katika singo hiyo, amewashirikisha mastaa kadhaa wa muziki Afrika wakiwemo, Tiwa Savage, Patoranking, Reekado Banks na Kanis. […]

Oct 7, 2023 - 13:00
 0
Lavauda awapa shavu Tiwa Savage, Kanis, Reekado Banks&Patoranking kwenye Roll on Me

Na Joseph Shaluwa

STAA wa kike kwenye uwezo mkubwa katika kuimba na kutunga, Lavaud amerejea kwa kishindo baada ya kuachia singo kali inayokwenda kwa jina la “Roll on Me” – ikiwa kwenye mitandao ya Saint & Citizen Music.

Katika singo hiyo, amewashirikisha mastaa kadhaa wa muziki Afrika wakiwemo, Tiwa Savage, Patoranking, Reekado Banks na Kanis.

Kwa hakika mastaa hao wamezidi kuinogesha singo hiyo na kuifanya yenye ladha ya kipekee.

Kwenye “Roll on Me” kuna mikono ya maprodyuza wakali, kama Kel-P, ambaye amepata kufanya kazi na wasanii Burna Boy, Wizkid, Rema na Trakmatik.

Akizungumzia traki hiyo, Lavaud anasema: “Nimefurahi sana kufanya kazi na wasanii wakubwa wenye uwezo na vipaji vya aina yake, lakini zaidi timu nzima ya utayarishaji. Nimependa jinsi tulivyoonyesha tamaduni na mila zetu za Kiafrika kwenye wimbo huo ambazo kwa hakika zimeongeza uzuri na upekee wa singo hiyo,” amesema.

Naye Tiwa Savage amesema: “Pale wasanii wanapokutana pamoja, kama hivi, kitu fulani cha kuvutia hutokea… na ndivyo ilivyokuwa.

“Huu wimbo ni mzuri na wa kipekee, nimefurahishwa na mchango wa kila mmoja wetu katika hii kazi,” amesema.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.