MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Wakati Serikali ikiwa imefunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika kuanzia Mei 15 hadi Agosti 15, mwaka huu, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa, Sultan Saleh Seif, ameruhusu wananchi kuendea la shughuli hizo. Seif alitoa kauli hiyo jana (June 26, 2024) wakati wa mkutano […]

Jun 27, 2024 - 19:00
 0
MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakati Serikali ikiwa imefunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika kuanzia Mei 15 hadi Agosti 15, mwaka huu, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa, Sultan Saleh Seif, ameruhusu wananchi kuendea la shughuli hizo.

Seif alitoa kauli hiyo jana (June 26, 2024) wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ninde, Kata ya Ninde wilayani Nkasi mkoani humo.

Itakumbukwa kuwa, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, akitangaza lengo la Serikali la kufunga kwa muda shughuli za uvuvi alisema lengo ni kupumzisha shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika kwa miezi mitatu ili kuwezesha samaki kuzaliana na kuongeza tija kwa wavuvi wanaofanya shughuli zao ziwani humo.

Kauli za Seif zilizonukuliwa katika video fupi inayozunguka mitandaoni, ikimnukuu MNEC huyo akihamasisha wananchi kuendea na shughuli za uvuvi, inatofautiana na sababu zilizotolewa na Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdalah Ulega ambaye alisema uamuzi wa Tanzania unatokana makubaliano yaliyoazimiwa katika kikao kilichofanyika mwaka 2022 kikihusisha nchi zinazozunguka ziwa hilo ambazo ni Zambia, Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Ulega alisema uamuzi huo ni utekelezaji wa Mkataba wa Kikanda wa Nchi Wanachama wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika unaoweka hatua na taratibu za usimamizi endelevu wa shughuli za uvuvi katika ziwa hilo.

Aliongeza uamuzi huo unatokana na utafiti uliobainisha kuwa kumekuwepo na upungufu mkubwa wa samaki na dagaa katika ziwa Tanganyika kunakotokana na ongezeko kubwa la uvuvi usio endelevu uliopelekea uharibifu wa mazalia ya samaki.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.