Serikali ya Tanzania kukutana na Mabalozi kujadili changamoto za kodi kwa Wawekezaji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imekubali ombi la mabalozi wa nchi mbalimbali la kuandaa kikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili wawekezaji kutoka nchi zao. Mabalozi walioomba kikao hicho ni pamoja na wale wa Marekani, […]

Jun 28, 2024 - 19:01
 0
Serikali ya Tanzania kukutana na Mabalozi kujadili changamoto za kodi kwa Wawekezaji
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imekubali ombi la mabalozi wa nchi mbalimbali la kuandaa kikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili wawekezaji kutoka nchi zao.

Mabalozi walioomba kikao hicho ni pamoja na wale wa Marekani, Uingereza, Uholanzi, Ufaransa, Ubelgiji, Canada, Korea, Sweden na Ujerumani.

Akijibu ombi hilo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, alisema serikali iko tayari kujadiliana na mabalozi hao kama walivyoomba, wakiamini kikao hicho kitakuwa na tija na kushughulikia changamoto zilizojitokeza.

“Nimekubali maombi yenu ya kikao kujadili changamoto mlizoziorodhesha na nitaandaa uwepo wa maafisa wa serikali kutoka taasisi husika kama mlivyoomba. Ili kikao kiwe na tija, tunaomba wawekezaji mnaowazungumzia waje na vielelezo vya kina vya changamoto zinazowakabili,” alisema Waziri Makamba.

Waziri Makamba aliwahakikishia mabalozi dhamira na nia dhabiti ya Serikali ya Awamu ya Sita kuendelea kuboresha mazingira ya kibiashara nchini, ili kuvutia uwekezaji kutoka nje (FDI). Alieleza kuwa serikali imefanikiwa kuongeza uwekezaji kutoka Dola za Kimarekani Bilioni 3 mwaka 2022 mpaka Bilioni 5.5 mwaka 2023.

Kikao hicho kinatarajiwa kuleta mwanga mpya katika juhudi za kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kuondoa vikwazo vinavyowakabili wawekezaji kutoka nje.

If you need to advertize with us contact us via whattsapp +254704208003
Unstoppable_ke My approach is characterized by meticulous attention to detail, critical thinking, and the ability to navigate the fine line between skepticism and empathy. I have honed skills such as data analysis, open-source investigation, undercover reporting, and source cultivation. My ability to maintain objectivity while delving into emotionally charged topics ensures that my work remains balanced and impactful.